Na Tiganya Vincent - RS-Tabora
SERIKALI imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na kiuhidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayazingatia vipaumbule vya Serikali na kuokuwa na manufaa kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni mkoani Tabora na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji na watumishi wa Mkoa huo.
Alisema kuwa mashirika hayapaswi kuanza kazi katika Halmashauri yoyote kabla ya mpango kazi wao hajaonwa na viongozi wa TAMISEMI ili kujidhirisha kama kweli malengo yao yanaendana na vipaumbele vya Serikali vya kuboresha maisha ya watanzana Watanzania ambao maisha yao yako chini.
Nzunda alisema baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakidai kusaidia Watanzania ,lakini matokeo yake ni kuwanufaisha viongozi wa mashirika hayo na wachache.
“Kwa mfano Mashirika hayo yanapokuja kutaka fulani kama vile elimu ni vema yakajua kuwa vipaumbele vya Serikali …….mfano kuboresha miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia, kuwajengea uwezo walimu, kuwepo na vifaa vya kufundishia na kuweka mazingira mazuri kwa watoto wenye mahitaji kujifunza na kusoma katika mazingira rafiki” alisema Nzunda
Alisema kuwa wanapoaandika taarifa kwenda kwa watu waliowawezesha fedha wanaonyesha kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli fedha nyingi zimeshia mifukoni kwa wachache na unapoenda katika eneo ambalo wanadai kusaidia hakuna kitu.
Nzunda alisema kuwa Serikali inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika na kama wafadhili wanapokuja waone kuwa fedha waliotoa imefanya kazi inayoonekana na sio maelezo yasiyo na ushahidi.
Alisema kuwa Serikali inapenda kushirikiana na wadau mbalimbali lakini ni vema wadau hao watambue kuwa vipo vipaumbele ambavyo inavikusudia katika kuwaletea maendeleo watu wake.
Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo ameagiza kuwa majengo yote yanayojengwa katika Shule na Taasisi mbalimbali za elimu yawe rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu na watoto wa kike ili kuondoa vikwazo vya wao kupata elimu.
Alisema kuwa baadhi ya majengo yamekuwa yakisababu wanafunzi wenye mahitaji maalumu kushindwa kuhudhiria masomo yao vizuri na kukwamisha ndoto zao za kuapata elimu.
Nzunda alisema kuwa yapo majengo ambayo yamekuwa hayana maeneo mazuri kwa ajili ya watoto wa kike na kuwafanya washindwe kuhudhuria masomo katika kipindi Fulani cha mwezi.