Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Yafanyika kwa Mara ya Kwanza.
May 31, 2019
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_43773" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akiwasili aktika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo kwa ajili ya hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Avemaria Semakafu na Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE, Profesa John Kondoro (kulia).[/caption]

Na Lilian Lundo - Dodoma.

Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mara ya kwanza limeandaa Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambayo yamefanyika Jijini Dodoma tarehe 27 hadi 30 Mei, katika uwanja wa Jamhuri.

Maonesho hayo yaliyofanyika kwa takribani siku tano na kufungwa leo na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ambapo kabla ya hotuba ya kufunga maonesho hayo, Ole Nasha aliweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo.

[caption id="attachment_43774" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Maonesho hayo yamehudhuriwa na zaidi ya Vyuo na Taasisi za Elimu zipatazo 100.[/caption] [caption id="attachment_43775" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE, Profesa John Kondoro akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Maonesho hayo yamehudhuriwa na zaidi ya Vyuo na Taasisi za Elimu zipatazo 100.[/caption] [caption id="attachment_43776" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Dkt. Adolf Rutayuga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Maonyesho hayo yamehudhuriwa na zaidi ya Vyuo na Taasisi za Elimu zipatazo 100.[/caption]

Ole Nasha amesema kuwa, maonesho hayo yametoa fursa kubwa kwa wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambapo wameweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vyuo na Taasisi na Ufundi za Elimu ya Mafunzo na Ufundi. Vile vile kufahamu huduma na bidhaa zinazotolewa na Taasisi hizo.

Vile vile amesema kupitia maonesho hayo Vyuo na Taasisi zilizoshiriki zimeweza kukutana pamoja na wadau hao, hivyo kupata fursa ya kujibu changamoto pamoja na kupokea ushauri kutoka kwa wadau wao.

Aidha amesema, maonesho hayo yametoa fursa kwa wanafunzi na wazazi kufahamu vyuo na masomo wanayotoa  pamoja na kupata ushauri wa chuo gani mwanafunzi anaweza kujiunga kutokana na ufaulu wake.

[caption id="attachment_43777" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo. Maonesho hayo yaliyoratitibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu.[/caption] [caption id="attachment_43778" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya kufunga maonyesho hayo leo Jijini Dodoma. Maonesho hayo yaliyoratitibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).[/caption] [caption id="attachment_43779" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akisistiza jambo alipotembelea moja ya banda la wanufaika wa Vyuo vilivyo chini ya usimamizi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo. Maonesho hayo yameratibiwa na NACTE). Kushoto ni Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Adnced Engeering Solutions Limited, Bi. Haika Lyimo.[/caption] [caption id="attachment_43780" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) – Hombolo, Profesa Madale Mpamile alipotembelea katika banda la Chuo hicho wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo leo Jijini Dodoma. Maonesho hayo yameratibiwa na NACTE).[/caption] [caption id="attachment_43781" align="aligncenter" width="750"] Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Kondoa, Bi. Daffi Damian akitoa huduma ya kupima mapigo ya moyo na presha kwa mwanchi aliyetembelea banda la Chuo hicho katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo. Maonesho hayo yameratibiwa na NACTE). Katikati ni Mwalimu wa Chuo hicho Bi. Esther Samwel[/caption] [caption id="attachment_43783" align="aligncenter" width="750"] Mwanafuzni wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Tecknology and Management (KITM) akielezea kuhusu teknolojia ya Atomotive ambapo unaweza kutumia simu ya mkononi kufunga na kufungua geti alipofanyiwa mahojiano maalum na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43784" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) mara baada ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo jijini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia , Dkt. Avemaria Semakafu, Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE, Profesa John Kondoro na Katibu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Dkt. Adolf Rutayuga.(Picha na: Frank Shija – MAELEZO)[/caption]

Ole Nasha ameitaka NACTE kuhakikisha maonesho hayo yanafanyika kila mwaka ili wadau wa elimu ya ufundi na mafunzo waendelee kunufaika na kupata uelewa wa shughuli zinazofanywa na vyuo na taasisi za elimu ya ufundi na mafunzo.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf Rutayuga amesema jumla ya Taasisi 100 zimeshiriki maonesho hayo ambapo kati ya Taasisi hizo 71 ni vyuo vya ufundi na mafunzo, 11 ni vyuo vikuu. 5 kampuni kupitia elimu ya mafunzo na ufundi na 13 ni kampuni za biashara.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda Tanzania.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi