Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makandarasi Kujadili Maendeleo ya Ukuaji wa Viwanda.
Oct 31, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21406" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi (CATA) Mhandisi Lawrence Mwakyambiki (katikati) akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) katika utambulisho wa mkutano wa chama hicho utakaofanyika Novemba 17, 2017 Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mauzo wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Bi.Kunenguda Dedede na kushoto ni Mkuu wa Masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa.[/caption]

Na: Paschal Dotto

Chama cha Makandarasi (CATA) kinachounganisha wakandarasi wote nchini kinatarajia kukutana Novemba 17, 2017 kujadili kuhusu ukuaji wa viwanda nchini mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumuza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhandisi Lawrence Mwakyambiki alisema kuwa  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli iko kwenye njia ya ujenzi wa viwanda kwa hiyo sekta ya ujenzi inahitajika kwa kiasi kikubwa kwenye sera hii ya viwanda.

“Lengo la mkutano huu kwa wakandarasi hawa ni kutaka kuleta mchango wao katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania na wameona kwamba kama wazawa wanaowajibu wa kutoa mchango katika katika ujenzi wa viwanda nchini”, alisema Mhandisi Mwakyambiki.

[caption id="attachment_21407" align="aligncenter" width="750"] Meneja Mauzo wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Bi.Kunenguda Dedede akieleza jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani) kuhusu mkutano wa makandarasi hapo novemba 17, 2017 katika ukumbi wa diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa na Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Tanzania (CATA) Mhandisi Lawrence Mwakyambiki.[/caption] Aidha Mhandisi Mwakyambiki alisema kuwa katika maendeleo ya taifa sekta ya ujenzi ni muhimu kwani inabeba vitu vingi na kuwawezesha wananchi kupata huduma stahiki kama elimu na afya, na kuwataka makandarasi kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.

Katika mkutano huu ambapo CATA watakuwa waratibu vyama vingine vya wakandaarasi vikiwemo Tanzania Civil Engineering Contractors Association(TACECA) pamoja na Association of Citizen Contractors(ACCT) na  mabenki  ya Benki ya Biashara Afrika (CBA) na NMB ambayo yatatoa ufadhili wa mkutano huo.

Akibainisha miradi itakayochukua nafasi katika majadiliano hayo Mwakyambiki alisema kuwa katika Serikali hii ya Awanu ya Tano miradi inayohitaji  wakandarasi ni Ujenzi wa miundombinu ya reli(SGR), sekta ya maji, bomba la kusafirisha mafuta ghafi (uganda – Tanzania) pamoja na ujenzi wa Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma.

Aidha aliongeza kuwa katika mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuliwa na wakandarasi zaidi ya 200 ambao watatoa mawazo yao kuelekea ujenzi wauchumi wa viwanda kama sera ya awamu ya tano inavyoelekeza  ni muhimu kwa ujenzi wa taifa.

Mhandisi Mwakyambiki alisema kuwa katika kutambua mchango wa wakandarasi ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kutokea Tanzania katika tasnia hiyo na mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa katibu mkuu wa sekta ya ujenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Injinia Joseph Nyamuhanga.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi