Makamu wa Rais, Waziri Mkuu Washiriki Kumuaga Mrema
Aug 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Doreen Kimbi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwafariji wanafamilia, viongozi na wanachama wa TLP alipofika msibani nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema walipofika msibani nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema kwenye Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohudhuria ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24, 2022.
Wafiwa na Viongozi wa Siasa wakiwa katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, baada ya ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24, 2022