Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Usafi Awamu ya Pili Dodoma
Dec 07, 2017
Na Msemaji Mkuu

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur wakikagua vyoo bora vinavyotumika na Wanafunzi wa shule ya Msingi  Humekwa,wilayani Chamwino mapema leo,ambapo Mh.Ummy amekagua usafi wa Mazingira pamoja na vyoo bora, ikiwa ni sehemu ya kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI'. 
 
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur wakiangalia  namna Kibuyu Chilizi kinavyosaidia kuepukana na magonjwa ya matumbo,kuhara pamoja na kipindupindu.
 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza mapema leo mbele ya Wanakijiji cha Humekwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma,na baadae kujibu kero kadhaa za wananchi huo kuhusiana sekta ya Afya katika kijiji hicho na kufanya ukaguzi wa Usafi wa Mazingira na Vyoo bora ikiwa ni sehemu ya kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira. 
Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur,ambaopia ni baadhi ya Wafadhiri wa Mazingira na Usafi katika sehemu mbalimbali hapa nchini,akiwasalimia baadhi wa wanakijiji cha Humekwa wilayani Chamwino,waliofika kwenye mkutano wa hadhara,ambapo mgeni rasmi alikuwa WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alifika katika kijiji hicho kukagua Usafi wa Mazingira na Vyoo bora kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI'., kulia ni Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dkt James Charles pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Vumilia Nyamonga. Mmoja wa Wanafunzi wa shule ya Msingi Humekwa,katika kijiji cha Humekwa wilayani Chamwino akinawa mikono kwa kutumia maji ya kibuyu chilizi pamoja sabuni mara baada ya kutoka chooni, kuepuka kuambukizwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo Kipindupindu. Baadhi ya wanakijiji cha Humekwa wilayani Chamwino,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara,ambapo mgeni rasmi alikuwa WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu ambaye amefika katika kijiji hicho kukagua Usafi wa Mazingira na Vyoo bora kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi