Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali waliofika nyumbani kwa marehemu Askofu Mstaafu, Gerald Mpango Boko Jijini Dar es salaam. Marehemu Askofu Mstaafu Gerald Mpango ni kaka wa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango. Januari 20, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na marehemu kaka yake Askofu Mstaafu, Gerald Mpango tarehe 16 Desemba 2021 wakati Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoani Kigoma. Askofu Mstaafu, Gerald Mpango alifariki jana tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam.