Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea maelezo ya eneo la mtambo wa kusafisha maji uliopo Loiborsoit Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati alipotembelea na kukagua mradi huo leo tarahe 15 Machi 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akicheza wimbo wa kabila la wamaasai wakati alipofika katika eneo la Loiborsoit kuweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa eneo la Loiborsoit mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.