Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango leo tarehe 13 Oktoba 2022 akisalimiana na baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila (mwenye shati jeupe) wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Makamu wa Rais anatarajia kuhudhuria sherehe za kilele cha mbio za Mwenge Kitaifa zitazofanyika mkoani Kagera na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 14 Oktoba, 2022.