Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Atoa Rai kwa Watanzania Kutoa Ushirikiano kwa Makarani wa Sensa
Aug 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 23 Agosti, 2022 ameshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambapo yeye pamoja na familia yake wamehesabiwa katika makazi yao Kijiji cha Zogowali kata ya Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi hilo, Makamu wa Rais ametoa rai kwa watanzania wote kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa ili waweze kupata taarifa sahihi zitakazowezesha Serikali kupanga vema maendeleo. Amesema zoezi la sensa ni wajibu wa kila mtanzania, hivyo inapaswa kufanywa kwa uadilifu mkubwa.

Makamu wa Rais amesema amefurahishwa na maswali yanayoulizwa katika zoezi hilo ambayo yanalenga huduma muhimu za kijamii zinazopatikana katika maeneo ya wananchi ili kuiwezesha Serikali kutambua huduma zinazokosekana katika maeneo hayo na uhitaji wake.

Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi limeanza rasmi leo tarehe 23 Agosti, 2022 na kuendelea kwa siku saba huku tarehe 23 ikiwa ndio tarehe rejea kwa ajili ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa kwa makarani wa sensa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi