Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwasili katika eneo la Upper Hill Nairobi nchini Kenya kukagua kiwanja cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachotarajiwa kujengwa jengo la Ghorofa 23 la Ubalozi na kitega uchumi cha Ubalozi,leo tarehe 4 Machi 2022
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akipokea maelezo juu ya mradi wa kitega uchumi cha Ubalozi wa Tanzania unaoatarajiwa kujengwa katika eneo la Upper Hill Nairobi nchini Kenya kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, John Simbachawene leo tarehe 4 Machi 2022