Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Aongoza Watanzania Mechi ya Everton Taifa
Jul 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6415" align="aligncenter" width="1000"] Wachezaji wa timu za Everton ya nchini Uingereza na Gor Mahia ya Kenya wakiingia Uwanjani kwa ajili ya kuanza mechi yao ya kirafiki iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam. Mchezo umemalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1.[/caption]

Na Shamimu Nyaki

Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, aliwaongoza maelfu ya Watanzania kushuhudia mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu za Everton FC ya Uingereza na Gor Mahia ya Kenya iliyochezwa jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mbali na Makamu wa Rais, viongozi nwengine walioshuhudia pamombano hilo ni pamoja na Marais Wastaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mzee Ali Hassan Mwinyi. Viongozi wengine ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Balozi wa Uingerenza Nchi, Bi. Sarah Cook, Makatibu Wakuu wa Wizara, Rais Mtaafu wa Shirikisho la Soka Tanzania, Leodigar Tenga na viongozi mbalimbali.

[caption id="attachment_6416" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiingia katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kukagua wachezaji wa timu ya za Everton na Gor Mahia ya nchini Kenya alipokuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo leo Jijini Dar es Salaam. Mchezo umemalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.[/caption] [caption id="attachment_6417" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua wachezaji wa timu ya Everton alipokuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya timu hiyo na Gor Mahia ya nchini Kenya mchezo ambao umechezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa magoli 2 -1. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa. Elisante Ole Gabriel.[/caption] [caption id="attachment_6421" align="aligncenter" width="908"] Wachezaji wa Timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya wakishangilia mara baada ya kusawazisha goli katika mechi ya kirafiki dhidi ya Everton FC iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam,Tanzania leo. Mchezo huo ulimalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1.[/caption]

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, ulishuhudia mchezaji Galacha wa Everton ambaye amesajiliwa kutoka klabu yake Manchester United, Wayne Rooney akiiandikia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 34.

Rooney alifunga goli hilo linalofanana kabisa na lile aliloifungia timu ya Everton dhidi ya Arsenal mwaka 2002 na kuamsha furaha ya mashabiki ambao kwa mara ya kwanza walimshuhudia mchezaji huyo akicheza katika ardhi ya Tanzania.

Hata hivyo goli hilo halikudumu kwani mnamo dakika ya 37 Jacques Tuyisenge aliisawazishia Gor Mahia na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.

[caption id="attachment_6420" align="aligncenter" width="1000"] Mchezaji wa Timu ya Everton FC Wayne Rooney (aliyenyoosha mikono) akishangilia goli mara baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika mechi ya kirafiki iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam,Tanzania leo. Mchezo huo ulimalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1.[/caption] [caption id="attachment_6419" align="aligncenter" width="1000"] Wachezaji wa timu za Gor Mahia na Everton FC wakigombea mpira wakati wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Tanzania leo. Mchezo umemalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1.[/caption] [caption id="attachment_6418" align="aligncenter" width="1000"] Mchezaji wa timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Everton FC wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Tanzania leo. Mchezo umemalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1.[/caption]

Katika kipindi cha pili timu ya Everton ilibadilisha kikosi chote ambapo kikosi hichi kilifanbya mashambulizi ya mara kwa mara loangoni mwa Gor Mahia na katika dakika ya 71 mchezaji kinda wa Everton, Kieran Dowell aliipatia timu yake goli la pili na kuifanya Everton kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Pamoja na kufungwa, timu ya Gor Mahia ilionesha uwezo mkubwa kwa muda wote wa mchezo ambapo wachezaji wake walionekana kutulia na kucheza kwa kuelewana na kumiliki mpira bila kujali majina makubwa ya wachezaji waliocheza nao kama Wayne Rooney, Garreth Barry, Aaron Lennon na wengine maarufu katika ligi kuu ya Uingereza.

[caption id="attachment_6422" align="aligncenter" width="531"] Mmoja wa mashabiki akiwa maemkumbatia mchezaji nyota wa Timu ya Everton FC Wayne Rooney baada ya kushindwa kuzuia kiu yake ya kushikana na mchezaji huyo na hatimaye kuamua kuingia katika ya uwanja na kufanya tukio hilo wakati wa mechi ya kirafiki baina ya timu hiyo na Gor Mahia ya nchini Kenya mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam leo. Mchezo huo ulimalizika kwa Everton FC kuibuka kidedea kwa jumla ya magoli 2 -1. (Picha zote na: MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi