Ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 yenye uwezo wa kupakia abiria 181 ikiwasili nchini kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam.na kumwagiwa maji (water salute) leo tarehe 03 Oktoba 2023.
Na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria kupokea ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Oktoba 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika ndege mpya ya abiria aina ya Boeing 737- MAX9 mara baada ya kuipokea ilivyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Oktoba 2023.