Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Aongoza Maadhimisho Mei Mosi Arusha
May 01, 2024
Makamu wa Rais Aongoza Maadhimisho Mei Mosi Arusha
Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi ya Kimataifa ambayo Kitaifa imefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha tarehe 01 Mei, 2024.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa mshikamano (Solidarity) wakati wa sherehe ya Mei Mosi ambazo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha tarehe 01 Mei, 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi na wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi za Serikali na Binafsi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi ya Kimataifa ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha tarehe 01 Mei, 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Gazeti la Mfanyakazi Tanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi ya Kimataifa ambayo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha tarehe 01 Mei, 2024. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua gazeti la Mfanyakazi Tanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi ya Kimataifa ambayo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha tarehe 01 Mei, 2024.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi