Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Akutana na Mabalozi Mbalimbali
Nov 16, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_22718" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha,Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka nchi nne kwa nyakati tofauti ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais alianza kukutana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke ambapo Makamu wa Rais aliupongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na kusema Uingereza imekuwa ikiifadhili Tanzania katika miradi mbali mbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini alielezea kuridhishwa kwake na kasi ya uwekezaji kutoka Uingereza na kuelezea kwamba nia ya Uingereza ni kuongeza uwekezaji .

 

Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi wa Uingereza kuwa milango ipo wazi kuja kuwekeza kwa wawekezaji wa Uingereza na katika kuelekea Tanzania ya Viwanda mazingira ya uwekezaji yataboreshwa zaidi ili wawekezaji waje kwa wingi zaidi Tanzania.

Mara baada ya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles ambapo Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine alizungumzia azma kubwa ya Tanzania ni kuona vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua vinapungua ama kumalizika kabisa pia Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo kuwa Wanawake wamedhihirisha wakipewa nafasi katika Uongozi wa Kijamii ama wa Kisiasa wanaweza kuongoza, Wanawake sasa wamekuwa kwenye vikosi vya kulinda amani.

[caption id="attachment_22720" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_22733" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_22734" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipomtembelea kwa mazungumzo ofisini kwake,Ikulu jijini Dar es Salaam.[/caption]

Balozi wa Canada alimpongeza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu nchini ambapo pia alisisitiza kudumishwa kwa mahusiano na ushirikiano ulioanzishwa miaka 56 iliyopita.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikutana na Balozi mpya wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke ambapo Makamu wa Rais aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa jitihada zake za kusaidia maendeleo na kufadhili miradi mbali mbali ya maendeleo ,Makamu wa Rais alisema ushirikiano kati ya nchi mbili hizi umezidi kuimarika tangu kuanzishwa  na waasisi wa Mataifa haya.

Aidha Makamu wa Rais alimpongeza Rais wa China Mhe. Xi Jing Ping kupitia kwa Balozi Wang Ke kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC)

Balozi wa China nchini alimpongeza Makamu wa Rais kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendelea kudumisha mahusiano na kufanya kazi vizuri.

Pia Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Oman Mhe. Ali Al Mahruqinchi ambapo walifanya mazungumzo ya kawaida ambapo suala la kuimarisha uhusiano na ushirikiano lilichukua nafasi kubwa.

[caption id="attachment_22747" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Oman nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption] [caption id="attachment_22749" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo.[/caption] [caption id="attachment_22750" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi