Makamu wa Rais Akabidhi Malori Maalum kwa TANAPA Yaliyotolewa na REGROW
Aug 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa pamoja na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika viwanja vya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro leo tarehe 17 Agosti, 2022 katika hafla ya kukabidhi Malori maalum kwa TANAPA yatakayotumika katika kuboresha Miundombinu ya Utalii yaliotolewa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwaongoza viongozi, maafisa , askari na wananchi mbalimbali kuimba wimbo wa Taifa mara alipowasili katika viwanja vya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro leo tarehe 17 Agosti, 2022 katika hafla ya kukabidhi Malori maalum kwa TANAPA yatakayotumika katika kuboresha Miundombinu ya Utalii yaliotolewa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).