Makamu wa Rais Ahani Msiba wa Mtoto wa Rais Mstaafu Mwinyi
Sep 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha kaka yake Hassan Ali Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 mara baada ya kufika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Chukwani mjini Zanzibar leo tarehe 04 Septemba, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpa pole Mama Siti Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 mara alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Chukwani mjini Zanzibar leo tarehe 04 Septemba, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 04 Septemba, 2022 wakizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuhani msiba Chukwani Mjini Zanzibar kufuatia kifo cha Hassan Ali Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022.