Makamu wa Rais Afungua Maabara ya Afya ya Jamii Kilimanjaro
Jul 16, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dtk. Philip Mpango akizindua mnaramaalum unaoonesha kuanza kwa hospitali hiyo nahuduma zinazotolewa wakati alipofika HospitaliMaalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’otokufungua Maabara ya Afya ya Jamii ya Hospitalihiyo iliopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro leotarehe 16 Julai 2022. Kulia ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dtk. Philip Mpango akipanda mti katika Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto wakati alipofika kufungua Maabara yaAfya ya Jamii ya Hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. tarehe 16 Julai, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dtk. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Afya na Mkoa wa Kilimanjaro katika gari maalumu ambaloni maabara ya magonjwa ambukizi lililopo katika Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto iliyopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. tarehe 16 Julai, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dtk. Philip Mpango akifungua Maabara ya Afya ya Jamii Ngazi ya 3 ya Hospitali ya Kibong’oto iliopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro leo tarehe 16 Julai, 2022. Kulia ni Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu.
Muonekano wa Maabara ya Afya ya Jamii ya Hospitali iliyopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 16 Julai, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dtk. Philip Mpango akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maabara ya Afya ya Jamii Ngazi ya 3 ya Hospitali ya Kibong’oto iliyopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro leo tarehe 16 Julai, 2022. Kushoto ni mke wa Makamu wa Rais, Mama Mboni Mpaye Mpango na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Stephen Kagaigai.