Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Afanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa UN New York
Sep 22, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo (Tete a tete ) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Antonio Guterres , Mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.

Hii leo tarehe 22 Septemba, 2022 Makamu wa Rais akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaondelea nchini Marekani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi