[caption id="attachment_37110" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspecta Generali wa Polisi (IGP) Simon Sirro akifunga mafunzo kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa na wale wa Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa awamu ya kwanza yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption]
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na wale wa Makao Makuu ya Jeshi hilo wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kuchochea mageuzi yakiutendaji ndani ya Jeshi hilo kupitia huduma wanazotoa kwa wananchi.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa makamanda hao leo Jijini Dodoma, Mkuu wa Jeshi hilo Inspecta Generali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amesema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo makamanda hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kujiepusha vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na maadili .
[caption id="attachment_37111" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Viongozi kutoka Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa na wale wa Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa awamu ya kwanza yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.[/caption]“Kwa sasa ni matumaini yangu kuwa mtabadilisha mitizamo yenu na kutambua jukumu kubwa mlilopewa na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea “. Alisisitiza IGP Sirro
Akifafanua amesema kuwa mafunzo hayo ni chachu yakuleta mabadiliko ndani ya Jeshi hilo ambalo ni taswira ya Serikali kwa wananchi.
Aliongeza kuwa makamanda hao wanalo jukumu kubwa la kusimamia sheria katika mikoa yao na kuhakikisha kuwa wale walio chini yao wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu.
[caption id="attachment_37113" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspecta Generali wa Polisi (IGP) Simon Sirro akiteta jambo na Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Viongozi kutoka Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Sing oleo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo.[/caption]Pia aliomba Taasisi ya Uongozi kuona umuhimu wa kuendelea kutoa mafunzo kwa maofisa wengine wa Jeshi hilo kwa kuzingatia maombi yakuwaptaia mafunzo hayo maofisa wasiopungua 200.
Aliongeza kuwa Polisi wana jukumu kubwa la kulinda Dola hivyo mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka na yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza tija.
Kwa upande wake , Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Viongozi kutoka Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza weledi na kuimarisha utendaji kwa Makamanda hao.
Taasisi ya Uongozi imekuwa ikiendesha mafunzo yakuwajengea uwezo Watendaji mbalimbali wa Serikali ili kuongeza tija na kuimarisha utendaji.
Mafunzo hayo yalijikita katika kuimarisha utendaji wa Makamanda hao, kujitambua, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, rushwa, muundo wa dola na mengine yaliyolenga kuimarisha na kuongeza tija ndani ya jeshi hilo.
[caption id="attachment_37114" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspecta Generali wa Polisi (IGP) Saimon Sirro akiwa kwenye picha ya pamoja na Sehemu ya Makamanda wa Polisi wa mikoa walioshiriki katika mafunzo ya siku tano yaliyofanyika Jijini Dodoma.