Majaliwa Azungumza na Viongozi Mbalimbali Nchini DRC
Feb 25, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa anayeshughulikiwa masuala ya amani, Jean-Pierre Lacroix baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kumi wa Wakuu wa Nchi wa Serikali zinazohusika na mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano nchini DRC na kwenye ukanda wa maziwa makuu uliofanyika, jijini Kinshasa, DRC Februari 24, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi katika mkutano wa pembeni baada ya kumalizika kwa mkutano wa Kumi wa Wakuu wa Nchi wa Serikali zinazohusika na mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano nchini DRC na kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika, jijini Kinshasa, DRC Februari 24, 2022.