Majaliwa Azungumza Katika Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Oct 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Msaada wa Kisheria (LSF), Lulu Ng’wanakilala kuhusu machapisho mbalimbali yanayotolewa na Asasi hiyo katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma , Oktoba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima Tuzo kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Oktoba 4, 2022. Katikati ni Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Mwantumu Mahiza kulia ni Mwenyekiti wa NaCONGO, Dkt. Lilian Badi
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Oktoba 4, 2022.