Majaliwa Azindua Vituo vya Kurushia Matangazo ya Radio TBC Taifa na TBC Fm
Apr 14, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakiwashuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashimba wakikabidhiana hati za vituo vya kurushia matangazo ya Radio TBC Taifa na TBC fm kwenye maeneo ya Ngara (Karega), Mlimba (Morogoro) Ludewa (Njombe) na Ruangwa (Lindi), Aprili 14, 2022 Ruangwa mkoani Lindi.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba (Kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashimba (Kushoto) wakikabidhiana hati za vituo vya kurushia matangazo ya Radio TBC Taifa na TBC fm kwenye maeneo ya Ngara (Karega), Mlimba (Morogoro) Ludewa (Njombe) na Ruangwa (Lindi), Aprili 14, 2022 Ruangwa mkoani Lindi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mhandisi Upendo Mbelle (Kushoto) wakati akimpa maelezo kuhusu mtambo uliopo kwenye kituo cha kurushia matangazo ya Radio TBC Taifa na TBC fm kilichopo Ruangwa (Lindi), Aprili 14, 2022 Ruangwa mkoani Lindi. Wa pili Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashimba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua vituo vipya vya kurushia matangazo ya Radio TBC Taifa na TBC fm kwenye maeneo ya Ngara (Karega), Mlimba (Morogoro) Ludewa (Njombe) na Ruangwa (Lindi), Aprili 14, 2022 Ruangwa mkoani Lindi.