Majaliwa Azindua Ugawaji wa Vishikwambi kwa Sekta ya Elimu
Nov 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kulia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu wakiwa wamebeba vishikwambi walivyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kutoka kulia ni Mwalimu Hadikwa Chidumizi wa Shule ya Msingi Nkuhungu Dodoma, Mwalimu Victoria Kishiwa wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwalimu Mashaka Mnjalloh, Mdhibiti wa Ubora wa Elimu katika jiji la Dodoma, Mwalimu Robert Tesha, Afisa Elimu Kata ya Mnadani Dodoma na kulia ni Mwalimu Bernard Sinkamba ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mnguru.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kishikwambi Mwalimu Bernard Sinkamba ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Munguri Dodoma wakati alipozindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Adolf Mkenda.