Majaliwa Azindua Programu ya Ajira kwa Vijana Kupitia Sekta ya Kilimo
Aug 03, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mche wa mgomba wakati alipotembelea banda la TAHA katika Maonyesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, Agosti 3, 2022. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na kushoto ni Bwana Shamba Kiongozi wa TAHA, Giliard Daniel.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ng'ombe wa kisasa wakati alipotembelea banda la kampuni ya Highland Estates Limited katika Maonyesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 3, 2022. Kulia ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.