Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kagera, Septemba 19, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu), David Silinde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Karagwe, Septemba 19, 2021. Kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu), David Silinde.
Marumaru zisizo na viwango vinavyokubalika Serikalini ambazo zimewekwa kwenye sakafu ya Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya wilaya ya Karagwe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amegiza ziondolewe na badala yake ziwekwe marumaru zenye ubora unaokidhi viwango vya Serikali. Mheshimawa Majaliwa alitoa maagizo hayo wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo na kukagua ujenzi wake akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kagera, Septemba 19, 2021.