Majaliwa Awasili Seoul, Korea ya Kusini kwa Ziara ya Kikazi
Oct 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim. Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Korea ya Kusini wakati walipowasili kwenye hoteli ya Lotte iliyopo Seoul nchini humo Oktoba 24, 2022 kwa ziara ya kikazi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini, Mhe. Togolani Mavura wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon nchini Korea ya Kusini Oktoba 24, 2022 kwa ziara ya kikazi nchini.