Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Hassan Pazi ambaye ni fundi mkuu wa kiwanda cha kuchenjua madini ya dhahabu cha Kampuni ya Giant ya Chunya mkoani Mbeya kuhusu uchenjuaji madini ya dhahabu wakati alipotembelea kiwanda hicho, Novemba 29, 2021. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Abdallah Kitwala
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuchenjua madini ya dhahabu cha Kampuni ya Giant ya Chunya mkoani Mbeya Novemba 29, 2021. Aliyekaa kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI, Dkt Festo Dugange na kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga, wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homela, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Mchungaji Jacob Mwakasole
Wanakwaya wa kundi la Agano wakiimba wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kipoka wilayani Chunya, Novemba. 29, 2021.