Majaliwa Atembelea Eneo la Ujenzi wa Mji Mpya Serikali ya Korea
Oct 26, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma, Meshack Bandawe (kulia) wakizungumza na Msimamizi wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Serikali ya Korea, Bw. Lee Sang Rae (katikati) wakati walipotembelea mji huo kwenye eneo la Sejong Oktoba 26, 2022 kwa lengo la kupata uzoefu utakaosaidia kuboresha ujenzi unaoendelea wa Mji wa Serikali Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Msimamizi wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Serikali ya Korea, Bw. Lee Sang Rae (kushoto) kuteremka kwenye mnara uliomwezesha kuona eneo lote la ujenzi wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa mji huo lililopo Sejong, Oktoba 26, 2022 kwa lengo la kupata uzoefu utakaosaidia kuboresha ujenzi unaoendelea wa Mji wa Serikali Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wanaosimamia Ujenzi wa Mji Mpya wa Serikali ya Korea baada ya kuona eneo lote la ujenzi wa mji huo wakiwa kwenye mnara maalum, Oktoba 26, 2022. Mheshimiwa Majaliwa alitembelea Mji huo kwa lengo la kupata uzoefu utakaosaidia kuboresha ujenzi unaoendelea wa Mji wa Serikali jijini Dodoma, Oktoba 26, 2022.