Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Nchini Angola
Dec 09, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, walipokutana katika Ukumbi wa Kimataifa wa Interconinental mapema kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiaya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika Angola jijini Luanda, Disemba 9, 2022.Waziri Mkuu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, pamoja na viongozi wengine kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia hoja zinazotolewa katika Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiaya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika nchini Angola Disemba 9, 2022.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiaya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika nchini Angola Disemba 9, 2022.