Majaliwa Amuwakilisha Rais Samia Katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran
Aug 14, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti mshindi wa kwanza wa kusoma na kuhifadhi Quran (Riwayat Warsh), Murtado Katibi kutoka Nigeria, wakati alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mashindano ya kimataifa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu, yaliyofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco na Makao Makuu wa Bakwata, Dar es Salaam, Agosti 14, 2022. Mashindano hayo yanafadhiliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI Ulamaa wa Afrika
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mfalme Mohamed VI Ulamaa wa Afrika, Mohamed Rifk alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mashindano ya kimataifa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu, yaliyofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco na Makao Makuu wa Bakwata, Dar es Salaam, Agosti 14, 2022. Mashindano hayo yanafadhiliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI Ulamaa wa Afrika
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, wakati alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mashindano ya kimataifa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu, yaliyofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco na Makao Makuu wa Bakwata, Dar es Salaam, Agosti 14, 2022. Mashindano hayo yanafadhiliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI Ulamaa wa Afrika.