Majaliwa Akutana na Rais wa AFRECO, Waonesha Nia Kusaidia UDOM, Akutana na Viongozi wa Makampuni ya Japan Yaliyowekeza Tanzania
Aug 29, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Association of African Economic Development (AFRECO), Bw. Tetsuro Yano, katika mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa TICAD uliofanyika jijini Tunis, Tunisia Agosti 28, 2022. Kampuni ya AFRECO imeonesha nia ya kujenga chuo cha Uhandisi wa Tiba (school of medical engineering) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kupunguza tatizo la wataalamu wa tiba na vifaa tiba nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Japan Tobacco Inc ya Nchini Japan, Bw. Mutsuo Iwai ambao ni wamiliki washirika wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) katika Mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa TICAD uliofanyika jijini Tunis, Tunisia, 28 Agosti, 2022.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mitsubishi Yasuteru Hirai, katika Mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa TICAD uliofanyika jijini Tunis, Tunisia, 28 Agosti, 2022. Katika mazungumzo yao, Mhe. Majaliwa ameiomba Kampuni hiyo kujenga kiwanda cha kuunganisha magari Tanzania.