Majaliwa Akagua Ujenzi wa Reli ya Kisasa Kipande cha Mwanza - Isaka
Oct 16, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Baadhi ya wananchi na viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha Isaka - Mwanza cha Reli ya Kisasa (SGR) katika Stesheni ya Fela mkoani Mwanza, Oktoba 16, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kipande cha reli cha majaribio wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa kipande cha Isaka - Mwanza cha Reli ya Kisasa (SGR) katika Stesheni ya Fela mkoani Mwanza, Oktoba 16, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Amina Lumuli.
Muonekano wa eneo katika Stesheni ya Fela kwenye ujenzi unaoendelea wa kipande cha reli ya Kisasa ( SGR) cha Mwanza-Isaka ambacho Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua Ujenzi wake, Oktoba 16, 2022.