Majaliwa Akagua Ujenzi wa Mradi wa Stendi Kuu ya Mabasi Nyegezi na Maendeleo ya Ujenzi wa MV Mwanza
Oct 18, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa mradi wa ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi Nyegezi jijini Mwanza, Mhandisi Henry Joseph (kushoto) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo jijini, Oktoba 17, 2022.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama michoro ya jengo la Stendi Kuu ya Mabasi Nyegezi jijini Mwanza, Oktoba 17, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima na kulia ni Mhandisi wa mradi huo, Henry Joseph
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Miradi wa Ujenzi wa Meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Vitus Mapunda (kulia) wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa meli hiyo kwenye Bandari ya Mwanza South jijini Mwanza, Oktoba 17, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya GESENTEC ya Korea Kusini, Dongmyung Kwak (kulia) kuhusu ujenzi wa Meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu wakati alipokagua Maendeleo ya ujenzi wa meli hiyo katika bandari ya Mwanza South jijini Mwanza , Oktoba 17, 2022.