Majaliwa Akagua Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Mwenge, Akagua ujenzi wa kingo za Mto Ng’ombe, Azungumza na Watumishi Wilayani Ilala
Jul 11, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Mwenge mkoani Dar es salaam akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kinondoni, Julai 11, 2022. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Mwenge mkoani Dar es salaam akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kinondoni, Julai 11, 2022. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar esalaam, Amos Mkala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa kingo za Mto Ng’ombe na mfereji wa Kiboko katika eneo la Tandale kwa Mtogole wilayani Kinondoni, Julai 11, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Wilaya ya Ilala, Wabunge na Madiwani kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Julai 11, 2022.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam na watumishi wa Wilaya ya Ilala wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Julai 11, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala baada ya kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam kwenye ukumbi wa Karimjee, Julai 11, 2022.