Majaliwa Akagua Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
Sep 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Asteria Shija baada ya kukagua ujenzi wa jengo la utawala la Manispaa hiyo ambalo ujenzi wake unasimamiwa vizuri na Mhandisi huyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Asteria Shija ambaye alitoa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wakati Waziri Mkuu alipokagua ujenzi wa jengo hilo, Septemba 8, 2022.
Hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la utawaa la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi huo, Septemba 8, 2022.