Majaliwa Akagua Ujenzi wa Chuo cha VETA Uyui Mkoani Tabora na Kubaini Madudu
Sep 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Nyumba ya walimu wa Chuo cha VETA Uyui mkoani Tabora ambayo imekadiriwa kujengwa kwa Shilingi milioni 114 na hadi sasa imetumia zaidi ya milioni 70. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikagua ujenzi wa Chuo hicho Septemba 8, 2022 aliagiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora isimamie ujenzi huo ili kudhibiti gharama kubwa zinazotumika katika ujenzi huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Chuo cha VETA Uyui mkoani Tabora, Septemba 8, 2022. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Batilda Buriani.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Chuo cha VETA Uyui mkoani Tabora. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake Septemba 8, 2022.