Majaliwa Afungua Mkutano wa Bunge Kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa
Mar 11, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Bunge kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2022/2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Machi 11, 2022. Kushoto kwake ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson katika Mkutano wa Bunge kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2022/2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Machi 11, 2022.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Machi 11, 2022
Baadhi ya Wabunge wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano wa Bunge kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2022/2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Machi 11, 2022.