Majaliwa Afungua Kongamano la 7 la Wahandisi Wanawake
Jul 29, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said tuzo ya mshindi wa kwanza ya Kiongozi Bora Mhandisi wa Kike wa Mwaka wakati alipofungua Kongamano la Saba la Wahandisi Wanawake kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es salaam, Julai 29, 2022.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhadisi Zena Ahmed Said, akionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza ya Kiongozi Bora Mhandisi wa Kike wa Mwaka aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati Waziri Mkuu alipofungua Kongamano la Saba la Wahandisi Wanawake kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es salaam, Julai 29, 2022. Katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Godfrey Kasekenya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mhandisi Consolata Ngimbwa tuzo ya mshindi wa kwanza Mkandarasi Bora Mhandisi wa Kike wa Mwaka wakati alipofungua Kongamano la Saba la Wahandisi Wanawake kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es salaam, Julai 29, 2022.