Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Magufuli, Makomandoo, Gwaride La Mkoloni Kupamba Sherehe Za Muungano
Nov 25, 2017
Na Msemaji Mkuu

 

Na: Jonas Kamaleki

Maadhimisho ya Sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatapambwa na Gwaride la Mkoloni, Makomandoo na Gwaride la kimyakimya ambapo Rais Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama katika mahojiano maalum na mwandishi wa habri hii.

Mhe. Mhagama alisema kuwa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatafanyika kitaifa mjini Dodoma, Makao Makuu ya Nchi, katika Uwanja wa Jamhuri.

Shughuli zitazofanyika siku hiyo ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama vikiwemo jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Polisi na Magereza, onesho la gwaride ya mkoloni, kwata ya kimyakimya na onesho la kikosi cha makomandoo.

Aidha, Mhe. Mhagama alisema kuwa kutakuwepo burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Ruvuma, Kigoma na Zanzibar, kwaya kutoka Chunya, Mbeya na burudani ya muziki kutoka kikundi cha Tanzania Allstars ikiwemo mziki wa kizazi kipya.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Uhuru wetu ni Tunu: Tuudumishe, Tulinde Raslimali zetu, Tuwe Wazalendo, Tukemee Rushwa na Uzembe”.

Mhe. Mhagama amezidi kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulinda rasilimali za nchi hasa madini.

“Vita ya kulinda rasilimali zetu iwe endelevu na ya kila mtu ili rasilimali hizo zimnufaishe kila mtanzania,” alisema Mhagama.

Aliwaomba wananchi wa mikoa ya Singida, Manyara, Morogoro, Dodoma na watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika Maadhimisho hayo ya kihistoria ambayo yataanza saa 12.00 asubuhi mjini Dodoma.

Ni mwaka wa 56 wa luadhimisha uhuru wa Tanzania Bara ambao ulikomesha utawala wa kikoloni wa Waingereza, uliopatikana Desemba 9, 1961 chini ya uongozishupavu wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi