[caption id="attachment_30693" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wakiwa kwenye majadiliano ya pamoja ambapo walizungumzia vipaumbele vinne, ikiwemo kuendeleza sekta ya viwanda pamoja na kukuza umoja wa kikanda katika sekta ya fedha na uwekezaji, mjini Washington DC Marekani.[/caption]
Na. WFM- Washington D.C
Benki ya Dunia (WB) imekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na athari za mafuriko zinazosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha kila mwaka katika Jiji la Dar es Salaam na kuleta madhara makubwa hususan katika eneo la Jangwani jijini humo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird, katika mikutano ya kipupwe inayoendelea mjini Washngton DC.
Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imekubali kusaidia kukabiliana na mafuriko katika bonde la mto Msimbazi hasa katika eneo la kutoka Magomeni Mapipa kwenda Faya na tayari Benki hiyo imeanza zoezi la kutafiti eneo la Jangwani ili kuweza kuangalia namna nzuri ya kugharamia uboreshaji wa mifereji katika bonde la mto Msimbazi ili kumaliza kero hiyo kwa wananchi wa Dar es Salaam.
[caption id="attachment_30694" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akisikiliza majadiliano katika mkutano wa SADC, ambapo alishauri katika utaratibu wa uandaaji wa bajeti ni vyema Mawaziri wa Fedha wakashirikishwa. Kushoto kwake ni Gavava wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, mjini Washington DC Marekani.[/caption]“Tumewaeleza Benki ya Dunia changamoto hii ambayo imekuwa inajirudia kila mara na kusababisha upotevu wa maisha ya watu, kusababisha kufungwa kwa barabara , watu kushindwa kwenda kazini na wanafunzi kushindwa kwenda shule, hivyo wameonesha nia ya kumaliza kero hii kwa wananchi “ Alisema Dkt. Mpango.
Amesema kuwa baada ya timu ya Benki ya Dunia kumaliza kufanya kazi yao kwa kushirikiana na Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, Serikali inaamini njia ya kudumu itapatikana na kuondokana na tatizo hilo la mafuriko ya mara kwa mara katika eneo la Jangwani.
[caption id="attachment_30695" align="aligncenter" width="800"] Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini majadiliano kati yake na Benki ya Dunia ya namna yakumaliza tatizo la mafuriko eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omar na wa kwanza kulia kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na wa pili kulia kwake ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere mjini, Washington DC Marekani.[/caption] [caption id="attachment_30696" align="aligncenter" width="800"] Ujumbe wa Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird. (upande wa kulia mwenye scarf shingoni) wakijadiliana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) namna ya kutatua changamoto za mafuriko eneo la Jangwani, mjini Washington DC Marekani. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)[/caption]