Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mafunzo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Wahasibu na Maafisa usimamizi wa fedha wa Mikoa wazinduliwa Mkoani Iringa
Jun 04, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya TEHAMA-TAMISEMI Bw.Baltazar Kibola akifuatilia jambo wakati wa  Mafunzo ya usimamizi wa fedha za umma kwa watumishi  wa mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa yaliyofanyika leo Mkoani Iringa.

Daudi Manongi- MAELEZO, Iringa

Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (epicor 10.2 utawajengea uwezo wahasibu na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa kusimamia vyema mapato na matumizi ya fedha za umma kwenye halmshauri zao.

Hayo yaesemwa leo Mkoani Iringa na Katibu tawala wa mkoa huo Bi Wamoja Ayubu wakati akifungua mafunzo ya mfumo huo  Mkoani hapa.

"Mfumo wa Epicor 10.2 umeandaliwa mahsusi kuungana na mifumo mingine ili kukidhi matakwa ya maboresho yanayoendelea, Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo ili muweze kusimamia fedha za umma na kuwapatia uelewa wa mabadiliko ya msingi yaliyofayika bila kukwamisha  utoaji wa huduma kwa wananchi" Alisema Bi.Ayubu

Aidha ameeleza kuwa kupitia mafunzo haya wahasibu na maafisa usimamizi fedha wa mikoa wataelekezwa kwa ufupi namna mfumo wa epicor 10.2 utakvyobadilishana taarifa na mifumo ya mipango na bajeti (PlanRep) pamoja na mfumo wa FFARS na hivyo kuleta utejelezaji wa dhana nzima ya uwazi,uwajibikaji  na  utawala bora katika usmamizi wa fedha za umma.

Muhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi.Catherine Kiyuo akimwelekeza jambo mshiriki wa mafunzo ya usimamizi wa fedha za umma kwa watumishi kwa watumishi wa mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa jinsi mfumo huo unavyofanya kazi leo Mkoani Iringa.

Washiriki wa Mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma ambao wanajumuisha wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo leo Mkoani Iringa.

Pamoja na hayo katibu tawala huyo ameishukuru TAMISEMI kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo ambao ni mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma(PS3), kwa kazi nzuri inayofaywa na mradi huo kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika  mkoani Iringa. Aidha amesema kuwa usimamizi wa fedha za umma unaendana na maboresho yanayoendelea ndani ya Serikali ambapo sasa Halmshauri zote pamoja na vituo vyake vya kutolea huduma zinatumia mifumo mingi zaidi  ya mfumo huu wa epicor kama mfumo wa ukusanyajo mapato na nk. Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi miundmbinu ya TEHAMA-TAMISEMI Bw.Baltazar Kibola amesema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI ilifanya maboresho makubwa kwa kuzifungia epicor toleo 9.05 halmshauri zote 133 zilizokuwepo wakati huo kupitia miundombinu ya TEHAMA iliyofungwa kwenye halmashauri zote na kusimamiwa na kampuni yasimu ya Taifa(TTCL), zoezi ambalo liliendelea kwa halmashauri mpya zilizoongezeka ambazo zilifungiwa epicor toleo namba 10.1.

Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha akielezea jinsi mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma ujulikanao kama Epicor 10.2 unavyofanya kazi kwa wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa mbalimbali leo Mkoani Iringa.

Aidha mafunzo haya yanafanyika katika vituo sita ambavyo ni Dodoma, Mwanza, Mtwara, Iringa, Kagera na Mbeya na kujumuisha watumiaji wa mfumo huo ambao ni waweka hazina,Wahasibu, maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa kwa awamu ya kwanza na maafisa Tehama, maafisa Manunuzi kwa awamu ya pili na wakaguzi wa ndani ambayo  yatafanyika baadae. Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara.  PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi