[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu katika ukumbi wa JKCI Dar es Salaam[/caption] [caption id="attachment_19945" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (kulia) Profesa Mohamad Janabi,na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Samuel Swai (kushoto) wakifuatilia mada na washiriki wakati wa Kongamano la nne kutoka mataifa mbalimbali duniani wakifuatilia jambo.[/caption]
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amefungua Kongamano la mafunzo ya Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu katika Ukumbi wa JKCI, Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa muda siku tano ambapo siku mbili ni za mafunzo yanadharia na siku tatu ni mafunzo kwa vitendo yatahusisha upasuaji.
Dkt. Mpoki amesema mafunzo yameratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Weil Cornel cha New York cha nchini Marekani, mafunzo hayo yamekuwayakifanyika kwa zaidi ya miaka 10 katika maeneo mbalimbali duniani ambapo hapa nchi yanafanyika MOI kwa mara ya nne.
Ili kuhakikisha mafunzo hayo yanaendelea kuwa na tija kwa taifa, Dkt. Mpoki amehahidi Serikali itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili mafunzo hayo yawe endelevu na yanawafikie madaktari wengi zaidi hapa nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Samuel Swai amesema Taasisi ya MOI imekuwa ikinufaika na mafunzo hayo kila mwaka ambapo wataalamu wake wamekuwa wakipewa mbinu mpya za upasuaji jambo ambalo limesaidia taasisi kupunguza idadi ya rufaa za wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu.
[caption id="attachment_19954" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt Mpoki Ulisubisya akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa MOI , Dkt Samuel Swai, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamad Janabi, Mratibu wa Mfunzo Dkt Hamis Shabani na Afisa Uhusiano wa MOI Patrick Mvungi.[/caption]Dkt. Swai amesema kutokana na mafunzo hayo Taasisi ya MOI imekuwa ikipokea misaada ya vifaa tiba mbalimbali ambavyo vimeweza kuwasaidia watanzania wengi.
Aidha, Dkt. Roger Hartl Mkurugenzi wa Kitengo cha upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka Chuo Kikuu cha Weil Cornel amesema ni heshima kubwa kufika Tanzania na ni faraja kwa mara nyingine kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na nchi nyingine duniani.
zaidi ya hayo, Dkt. Hartl amesema mafunzo ya mwaka huu yanalenga kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kutumia teknoljia ya kisasa ya matibabu ya Ubongo na mgongo na kuwapa mbinu mpya za upasuaji kwa mgonjwa aliyeumia kwenye eneo la mfumo wa fahamu hususan kwenye ubongo, uti wa Mgongo na mishipa ya fahamu iliyoharibika.
Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya madaktari 100 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Malawi, Namibia na nchi nyingine za Afrika. Mafunzo yanatolewa na Madaktari bingwa nane wazalendo kutoka MOI na wengine 15 kutoka nchini Marekani na Ulaya.