[caption id="attachment_47135" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.[/caption]
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kuitangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi. Joseph Nyamhanga alipokuwa akifunga mafunzo ya siku ya tano ya Uandishi wa Habari za Serikali kwa Usahihi kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali, leo Jijini Dodoma.
[caption id="attachment_47152" align="aligncenter" width="750"]"Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo makubwa sana ikiwemo ujenzi wa barabara za lami, madaraja, reli ya kisasa, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, utoaji wa elimu bila malipo, ununuzi wa ndege mpya pamoja na ujenzi wa jengo la tatu la abiria Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere," amesema Nyamhanga.
Amesema, Maafisa Mawasiliano wanalo jukumu la kutangaza miradi hiyo na mingine mingi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara (Habari) Jonas Kamaleki amesema mafunzo hayo ya siku tano yamehusisha uandishi wa kimkakati ya uandishi wa habari za Serikali kwa usahihi, namna ya kutengeneza taarifa za redio na televisheni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii.
[caption id="attachment_47153" align="aligncenter" width="750"]Aidha, Afisa Habari wa Halmashauri ya Bahi, Benton Nollo amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu sana kwao kama Maafisa Mawasiliano wa Serikali, amemuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano kuitangaza vyema miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo imehusisha zaidi ya Maafisa Mawasiliano kutoka Taasisi na Idara za Serikali, Wizara, Mikoa na Halmashauri za Wilaya.