Mhasibu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Noah Tambukwa akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) kwa Maafisa Manunuzi wa Halmashauri za Kigoma, Kasulu na Mkalama, leo Jijini Dodoma.
Maafisa Manunuzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Oscar Mshana (kushoto), Halmashauri ya Mji Shinyanga, Bw. Abraham Kimambo (katikati) na Halmashauri ya Bahi, Bi. Yaweaichiwake Macha (kulia) wakifanya mazoezi ya kutumia mfumo wa malipo (epicor 10.2), leo Jijini Dodoma. Mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa kuanzia Julai 1 mwaka huu ambapo utahusisha masuala yote ya fedha katika Mamlaka hizo ikiwa ni pamoja na mapato, matumizi pamoja bajeti ya Halmashauri husika.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi Manispaa ya Ubungo Bibi Azamah Ngwada (kushoto) na Afisa Manunuzi Halmashauri ya Ushetu, Bi. Elilight Mmari (Kulia) wakifanya mazoezi ya kutumia mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa Maafisa Manunuzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, leo Jijini Dodoma.
Afisa Manunuzi Msaidizi Halmashauri ya Longido Bi. Josephine Msuya akiuliza swali kuhusiana na mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa Maafisa Manunuzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, leo Jijini Dodoma.
(Picha na Lilian Lundo- MAELEZO, Dodoma )