[caption id="attachment_41392" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na Maafisa Habari wa Serikali wakati akifunga kikao cha 15 cha Maafisa hao leo Jijini Mwanza.Naibu Waziri uyo amewasisitiza maafisa hao kuyatangaza na kuyatetea mazuri ya Serikali ya Awamu ya Tano.[/caption]
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Maafisa Habari wa Serikali wamesisitizwa kuendelea kutangaza mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
[caption id="attachment_41386" align="aligncenter" width="1000"] Mhadhiri kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Dkt.Darius Mukiza akiwafundisha Maafisa mawasiliano wa Serikali tathmini ya utoaji wa habari za Serikali na maeneo ya kuonyeshwa mfano na changamoto za kufanyia zake leo Jijini Mwanza.[/caption]Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alipokuwa akifunga Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari wa Serikali kilichofanyika jijini humo kwa siku tano.
[caption id="attachment_41389" align="aligncenter" width="1000"] Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Bw.Titus Kaguo akitoa mada kuhusu Mbinu na jinsi ya Kuboresha Uhusiano na Vyombo vya Habari kwa Maafisa Habari wa Serikali katika Kikao cha 15 cha Maafisa hao leo Jijini Mwanza.[/caption]Bi Shonza amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mageuzi makubwa tangu iingie madarakani mwezi Novemba mwaka 2015 ambapo wananchi wameshuhudia mageuzi mbalimbali katika Sekta za Afya, Elimu, Maji, Usafiri wa Anga, Miundombinu ya Barabara, Reli na viwanja vya ndege.
[caption id="attachment_41393" align="aligncenter" width="1000"] Mtaalamu kutoka Wizara ya Afya Dkt Said Kanenda akizungumza na Maafisa Habari wa Serikali (hawapo pichani) juu ya Mtindo Bora wa maisha kiafya katika Kikao cha 15 cha Maafisa hao leo Jijini Mwanza.[/caption]“Mafanikio yote haya yanapaswa kuelezwa kwa wananchi, jukumu hilo ni la nyinyi Maafisa Habari wa Serikali hivyo ni imani yangu kuwa mafunzo na uzoefu mlioupata kupitia Kikao Kazi hiki yataleta chachu ya kutangaza zaidi shughuli za Serikali kupitia njia mbalimbali zikiwemo Televisheni, Magazeti, Tovuti pamoja na mitandao ya kijamii”, alisisitiza Bi Shonza.
[caption id="attachment_41390" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholas William akijadili jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Rodney Thadeus wakati wa kikao cha 15 cha Maafisa Mawasiliano Serikalini leo Jijini Mwanza.[/caption]Akifafanua kuhusu maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yaliyotolewa wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Naibu Waziri Shonza amesema kuwa maelekezo yaliyotolewa kwa viongozi wa Serikali na Maafisa Habari wa Serikali yamelenga katika kuboresha Sekta hiyo na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati juu ya utekelezaji wa Serikali hivyo ni lazima yazingatiwe na kutekelezwa.
[caption id="attachment_41391" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akichangia hoja wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali.[/caption]Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa kikao hicho kimehudhuriwa na takribani Maafisa Habari wa Serikali 400 ambao wamepata mafunzo kupitia mada mbalimbali zilizotolewa ambazo zimejikita katika kuboresha utekelezaji wa kada ya habari.
[caption id="attachment_41388" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Maafisa Mawasiliano Serikali wakifuatilia mada mbalimbali katika Kikao cha 15 cha Maafisa hao leo Jijini Mwanza.[/caption] [caption id="attachment_41384" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya Maafisa Mawasiliano Serikali wakifuatilia mada mbalimbali katika Kikao cha 15 cha Maafisa hao leo Jijini Mwanza.[/caption]“Kwa umoja wetu tumepata wasaa wa kutathmini na kuchambua mambo mbalimbali tunayopaswa kufanya na yale ambayo Serikali inatakiwa kufanya pia kwa kuwa hakuna muongozo wa matumizi ya mitandao ya kijamii, kupitia kikao kazi hiki tumejadili na kupata rasimu ambayo tutaiboresha na hivi karibuni Kada ya Habari itakua na muongozo wa kutumia mitandao ya kijamii”, alisema Dkt. Abbasi.
Miongoni mwa mambo yaiyojadiliwa ni pamoja na mbinu za medani za kihabari wakati wa dharura, Mwongozo wa maudhui mitandaoni, Mbinu na mkakati wa kuboresha uhusiano na vyombo vya habari, Usanifu wa lugha na uandishi mzuri wa taarifa kwa umma, Mbinu aushi za upigaji picha jongefu za habari na makala pamoja na habari za uongo katika kazi za Maafisa Habari na Mikakati ya Kukabiliana nazo.