Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani Kitaifa Yafana Manyara
Jul 20, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, iliyofanyika kitaifa wilayani Hanang’, mkoani Manyara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye, wakiangalia alizeti iliyozalishwa kwa kutumia mbegu ya kisasa wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, iliyofanyika kitaifa wilayani Hanang’, mkoani Manyara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akicheza ngoma ya kikundi cha utamaduni cha kabila la Kiiraq cha Gehandu kutoka Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Watu Duniani, iliyofanyika kitaifa wilayani Hanang mkoani Manyara.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, wakifurahia jambo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa wa Wizara hiyo, Bw. Royal Lyanga, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, iliyofanyika wilayani Hanang’, mkoani Manyara.