Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Lugola Aiagiza DUWASA Kuelimisha Wananchi Kutotumia Maji Taka
Feb 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="871"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola akimsikiliza (Mwenye Traksuti) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) Mhandisi David Pallangyo alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji wa Mamlaka hiyo mapema leo wakati wa ziara yakukagua miundo mbinu ya Maji taka katika Mjini wa Dodoma yakiwemo mabwawa ya kutunzia maji taka.[/caption]   [caption id="attachment_28739" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola (Mwenye Traksuti) akionesha athari za uchafuzi wa mazingira katika eneo lenye mabwawa ya maji taka yaliyopo Swawa, mjini Dodoma wakati wa ziara yake katika eneo hilo mapema leo, Mabwawa hayo yanasimamiwa na kuendeshwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA).[/caption]

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Mazingira Kangi Lugola ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya mabwawa yanayohifadhi maji taka kutoyatumia maji hayo kwa kilimo au matumizi yoyote ya nyumbani.

Lugola ametoa agizo hilo leo, mjini Dodoma alipofanya ziara katika mabwawa yanayohifadhi maji taka yaliyopo maeneo ya Swaswa, ambapo wananchi wa maeneo hayo wameonekana wakiyatumia maji hayo katika kilimo na wengine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani.

"Mnapofungulia maji taka kutoka katika mabwawa hakikisheni mnaweka ulinzi wa kutosha ili maji taka hayo yasielekezwe kwenye mashamba na makazi ya watu," alisema Lugola.

[caption id="attachment_28741" align="aligncenter" width="750"] Moja ya Mabwawa yanayotumika kuhifadhi maji taka katika eneo la Swaswa mjini Dodoma kama linavyoonekana.[/caption] [caption id="attachment_28742" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola (Mwenye Traksuti) akionesha jinsi kutokuzingatiwa kwa Kanuni za utunzaji wa maji taka katika mabwawa ya DUWASA kulivyochochea uharibifu wa mazingira ikiwemo kuathiri shughuli za maendeleo kama ujenzi kwa wamiliki wa viwanja vilivyopo jirani na eneo hilo.[/caption]

Aidha amemtaka Mkurugenzi Mkuu  wa DUWASA  kuhakikisha kuwa ana kibali cha kutiririsha maji taka kutoka bonde la mto Wami-Ruvu, vile vile maji hayo yawe yametibiwa na kutiririshwa kwa kiwango kinachotakiwa.

Pia ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha mabwawa mawili ambayo hayatumiki kuhifadhi maji taka yanafufuliwa na kutumika kufikia tarehe 31/12/2018 ili kukidhi idadi ya watu inayoongezeka mkoani Dodoma kutokana na Makao Makuu ya Nchi kuhamia mkoani humo.

[caption id="attachment_28746" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Taka na Maji Safi Dodoma (DUWASA) Mhandisi David Pallangyo akimueleza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Kangi Lugola jinsi wananchi wanavyochepusha maji taka nyakati za usiku kutoka katika mabwawa yakuhifadhi maji hayo na kuyatumia kwa shughuli za Kilimo hali inayochochea uharibifu wa Mazingira. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma) [/caption]

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa DUWASA Mhandisi David Pallangyo amesema ameyapokea maagizo ya naibu waziri huyo, ikiwa ni pamoja na kuyafufua mabwawa mawili ambayo yalikuwa hayatumiki ili kukidhi ongezeko la watu mkoani humo.

Hata hivyo amesema, mamlaka hiyo ipo katika mpango wa kujenga mabwawa ya kisasa katika eneo la Nzuguni ambalo litakidhi na kuendana na ongezeko la watu katika mkoa wa Dodoma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi