Korea Yaipatia Tanzania Mkopo Nafuu - Majaliwa Ashuhudia Utiaji Saini
Oct 27, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Tanzania na Korea leo Oktoba 27, 2022 zimetia saini mikataba miwili ambapo Korea itaipatia Tanzania mkopo nafuu wa Shilingi bilioni 310 kupitia Benki ya Exim ya Korea. Mikataba hiyo inahusu awamu ya pili ya upanuzi wa mfumo wa utambuzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Shilingi bilioni 161 mwingine ni Uendelezaji na Utunzaji wa Mfumo wa Taarifa za Ardhi Shilingi bilioni 149. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu wa Korea, Han Duck – Soo walishuhudia utiaji saini huo. Pichani, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mpango, Emmanuel Tutuba (kushoto ) na Hee-seong Yoon, Rais wa Benki ya Exim ya Korea wakipongezana baada ya kutia saini mikataba hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Korea iliyopo Seoul, Oktoba 27, 2022.
Tanzania na Korea leo Oktoba 27, 2022 zimetia saini mikataba miwili ambapo Korea itaipatia Tanzania mkopo nafuu wa Shilingi bilioni 310 kupitia Benki ya Exim ya Korea. Mikataba hiyo inahusu awamu ya pili ya upanuzi wa mfumo wa utambuzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Shilingi bilioni 161 mwingine ni Uendelezaji na Utunzaji wa Mfumo wa Taarifa za Ardhi Shilingi bilioni 149. Pichani, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu wa Korea, Han Duck – Soo ( kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mpango, Emmanuel Tutuba (wa pili kulia) na Hee-seong Yoon, Rais wa Benki ya Exim ya Korea (wa pili kushoto) baada ya kutiwa saini mikataba hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Korea iliyopo Seoul, Oktoba 27, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Korea, Han Duck Soo kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu huyo iliyopo Seoul, Oktoba 27, 2022.