Katibu wa Kikosi kazi cha kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akieleza jambo kwa wajumbe wa kikosi kazi hicho hiyo walipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali.
Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiweka nguzo ya umeme katika eneo la Ihumwa ambalo limetengwa kwa ajili ya mji wa serikali Dodoma.
Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Nigel Msangi akipata maelezo ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi kazi kutokana na ramani ya Mji wa Serikali walipotembelea kukagua eneo hilo Ihumwa, Dodoma. [caption id="attachment_32871" align="aligncenter" width="750"] Afisa Mipango Miji Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw.William Alfayo akiwaonesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea eneo hilo Juni 7, 2018[/caption] Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakiangalia maeneo mbalimbali yaliyotengwa kulingana na ramani ya Mji mpya wa Serikali Ihuma Dodoma.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)