Na Mwandishi Wetu, TANGA
Kikao Kazi na Mafunzo kwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini kimeanza leo tarehe 4 April 2022 mkoani Tanga.
Kikao hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
Katika kikao hicho pamoja na uwasilishwaji mada, Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini watapata mafunzo ya namna bora ya kuendesha mashauri ya ardhi pamoja na uandishi mzuri wa hukumu.
Katika siku ya kwanza ya kikao hicho Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud aliwasilisha mada kuhusiana na masuala mtambuka katika uendeshaji mashauri ya ardhi.
Kikao hicho cha siku nne kinatarajiwa kumalizika siku ya alhamisi tarehe 7 April 2022.